Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema:

Available in 61 languages
«Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mazuri, na Akhera mazuri, na utukinge na adhabu ya moto".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikithirisha dua kwa dua fupi zenye kukusanya mambo mengi, na miongoni mwake: "Ewe Mwenyezi Mungu! Tupe hapa katika Dunia (mambo) mazuri, na Akhera utupe mazuri na utukinge na adhabu ya moto", Dua hii inakusanya mazuri yote ya Dunia; ikiwemo riziki ya raha na pana na ya halali, na mke mwema, na mtoto kitulizo cha jicho, na starehe, na elimu yenye manufaa, na mfano wa hayo miongoni mwa maombi yanayopendeka na ya halali, na mazuri ya Akhera ni kusalimika na adhabu za kaburi, na kisimamo cha Kiyama na moto, na kupata radhi za Mwenyezi Mungu, na kufaulu kwa kupata neema za kudumu, na kuwekwa karibu na Mola Mlezi Mwingi wa huruma.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality