Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Kutoka kwa Ubaidillaah bin Mihswan Al-Answari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:

Available in 47 languages
«Kutoka kwa Ubaidillaah bin Mihswan Al-Answari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayeamka miongoni mwenu akiwa na afya njema katika mwili wake, akiwa na amani katika mji wake, na anamiliki chakula cha siku yake hiyo, basi atakuwa ni kama kakusanyiwa dunia (yote)".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba atakayeamka miongoni mwenu enyi waislamu akiwa mzima wa afya katika mwili wake akiwa amesalimika na matatizo na magonjwa, akiwa na amani ndani ya nafsi yake na watu wake na familia yake na barabara zake, na akiwa hana hofu, na akiwa na chakula cha halali cha kumtosha kwa siku yake; basi ni kana kwamba kakabidhiwa dunia yote nzima.

Source
Imepokelewa na Tirmidhi na bin Majah
Download image

Saved at original quality