Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Kutoka kwa Khaula bint Hakim As-Sulamiyya, amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:

Available in 66 languages
«Kutoka kwa Khaula bint Hakim As-Sulamiyya, amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayeshuka mahali akasema: Audhubikalimaatillaahit-taammaati min sharri maa khalaqa (Najilinda kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyotimia kutokana na shari ya vile alivyoviumba) hakitomdhuru kitu mpaka aondoke mahala pake hapo".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anauelekeza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake katika kushikamana na kukimbilia kwenye tija ambako hutoeka kila chenye kuogofya anachokiogopa mwanadamu pale anaposhuka mahali katika ardhi, sawa sawa awe safarini au matembezini na kwingineko: Kuwa ajikabidhi na atake ulinzi kupitia maneno ya Allah yaliyotimia katika fadhila zake na baraka zake na manufaa yake, yaliyosalimika na kila aibu na mapungufu, kutokana na shari ya kila kiumbe chenye shari, ili awe na amani katika mazingira yake hayo kwa muda wote atakaokuwa hapo kutokana na kila chenye kuudhi.

Source
Imepokelewa Imamu Muslim
Download image

Saved at original quality