Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Kutoka kwa Abdillah Bin Khubaibi Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye amesema:

Available in 60 languages
«Kutoka kwa Abdillah Bin Khubaibi Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye amesema: Tulitoka katika usiku wa mvua kubwa na giza nene, tukimtafuta Mtume rehema na amani ziwe juu yake; ili atusalishe, anasema: Nikampata, akasema: "Sema" Nikawa sikusema kitu, kisha akasema: "Sema", Nikawa sikusema kitu, akasema: "Sema" Nikasema: Niseme nini? Akasema: "Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anaeleza swahaba mtukufu Abdullah Bin Khubaib radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa wao walitoka katika usiku wenye mvua kubwa, na giza lilikuwa nene, kwa ajili ya kumtafuta Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake; ili awasalishe, wakamkuta, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: "Sema" Yaani: Soma, akawa hakusoma kitu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akarejea kauli yake kwake, Abdullah akasema: Nisome nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Soma suratul Ikhlaswi (Qul-huwallaahu ahadi), na sura mbili za kinga (Qul-Audhubirabbil-falaq), na (Qul-Audhubirabbin-naas), wakati wa jioni, na wakati wa asubuhi, mara tatu tatu, zitakuhifadhi na kila shari, na zitakukinga na kila baya.

Source
Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
Download image

Saved at original quality