Hadith for the World
Fiq'hi yaDua na Dhikri mbali mbali.

Nyiradi za Asubuhi na Jioni.

4 hadiths

4 hadiths

عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: كان نبي الله صلى الله عليه وسلم إذا أمسى قال: «أمسينا وأمسى الملك لله، والحمد لله، لا إله إلا الله وحده لا شريك له» قال الراوي: أَرَاهُ قال فِيهِنَّ: «له الملك وله الحمد وهو على كل شيء قدير، ربِّ أسألك خير ما في هذه الليلة وخير ما بعدها، وأعوذ بك من شر ما في هذه الليلة وشر ما بعدها، رب أعوذ بك من الكسل، وسُوءِ الكِبَرِ، رب أعوذ بك من عذاب في النار، وعذاب في القبر»، وإذا أصبح قال ذلك أيضا «أصبحنا وأصبح الملك لله».رواه مسلم
Kutoka kwa Shadaad Bin Ausi Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Bwana wa Istighfari (Dua ya kuomba msamaha) Ni kusema: Allaahumma anta Rabbi Laa ilaaha illaa anta, khalaqtani wa anaa abduka wa ana a'laa a'hdika, wawa'dika mastatwa'tu, auudhubika min Sharri maa swana'tu, abuu ulaka bini'matika alaiyya, wa abuu ulaka bidhambi faghfirlii, fa innahuu laa yaghfirudh-dhunuuba illaa anta" Akasema: "Na atakayeisema dua hii mchana akiwa na yakini nayo, akafa katika mchana wake huo kabla hajafika jioni, basi atakuwa miongoni mwa watu wa peponi, na atakayeisema wakati wa usiku akiwa na yakini nayo, akafariki kabla hajafika asubuhi, basi huyo atakuwa miongoni mwa watu peponi".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Kutoka kwa Abdillah Bin Khubaibi Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye amesema: Tulitoka katika usiku wa mvua kubwa na giza nene, tukimtafuta Mtume rehema na amani ziwe juu yake; ili atusalishe, anasema: Nikampata, akasema: "Sema" Nikawa sikusema kitu, kisha akasema: "Sema", Nikawa sikusema kitu, akasema: "Sema" Nikasema: Niseme nini? Akasema: "Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu".Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesoma aya mbili za mwisho wa suratul Baqara zitamtosheleza".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake