Hadith for the World
Fiq'hi yaDua na Dhikri mbali mbali.

Adh-kaar zote - mbalimbali.

5 hadiths

5 hadiths

Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Dhikiri bora ni: Laa ilaaha Illa llaah: Na dua bora ni: Al-hamdulillah".Imepokelewa na Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah
عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : "الْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ، لَا إلَهَ إلَّا اللَّهُ، وَسُبْحَانَ اللَّهِ، وَاَللَّهُ أَكْبَرُ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إلَّا بِاَللَّهِ".رواه ابن حبان والحاكم، أما النسائي فرواه في الكبرى لكن من حديث أبي هريرة
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Maneno mawili mepesi mno katika ulimi, ni mazito mno katika mizani, yanapendeka mno kwa Al-Rahmani (Mwingi wa rehema) Ni: Sub-haanallahil Adhwiim, Sub-haanallaahi wabihamdihi".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kusema kwangu: Sub-haanallaah, na Alhamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allaahu Akbaru, kunapendeka sana kwangu kuliko vitu vyote vilizochomozewa na jua".Imepokelewa Imamu Muslim
عَنْ أَبِي مَالِكٍ الْأَشْجَعِيُّ عَنْ أَبِيهِ قَالَ: كَانَ الرَّجُلُ إِذَا أَسْلَمَ عَلَّمَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الصَّلَاةَ، ثُمَّ أَمَرَهُ أَنْ يَدْعُوَ بِهَؤُلَاءِ الْكَلِمَاتِ: «اللهُمَّ اغْفِرْ لِي وَارْحَمْنِي وَاهْدِنِي وَعَافِنِي وَارْزُقْنِي». وَفِي رِوَايَةٍ: أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَأَتَاهُ رَجُلٌ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ كَيْفَ أَقُولُ حِينَ أَسْأَلُ رَبِّي؟ قَالَ: «قُلْ: اللهُمَّ اغْفِرْ لِي وَارْحَمْنِي وَعَافِنِي وَارْزُقْنِي» وَيَجْمَعُ أَصَابِعَهُ إِلَّا الْإِبْهَامَ «فَإِنَّ هَؤُلَاءِ تَجْمَعُ لَكَ دُنْيَاكَ وَآخِرَتَكَ».رواه مسلم