Hadith for the World
Fiq'hi yaDua na Dhikri mbali mbali.

Muongozo wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na Amani katika kuleta Adhkaar- nyiradi.

5 hadiths

5 hadiths

ImepokelewaKutoka kwa Jabir radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, hakika yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Anapoingia mtu nyumbani kwake akamtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake na wakati wa chakula chake, Shetani husema: Hakuna malazi kwenu, wala chakula cha usiku, na anapoingia na hakumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake, Shetani husema: Mmepata malazi, na asipomtaja Mwenyezi Mungu wakati wa chakula chake, husema: Mmepata malazi na chakula cha usiku".Imepokelewa Imamu Muslim
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako nimejisalimisha, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako napambana. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kwa utukufu wako hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe najikinga kwa kuto nipoteza, wewe ndiye uliye hai ambaye hafi, na majini na watu wanakufa".Hadithi hii imepokelewa na Bukhari na Muslim, na matamshi haya ni ya Muslim, na akaipokea Bukhari kwa ufupi
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «وَاللهِ إني لأَسْتَغْفِرُ اللهَ وأَتُوبُ إليهِ في اليومِ أَكْثَرَ من سَبْعِينَ مَرَّةً».رواه البخاري
Kutoka kwa Agharri radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Enyi watu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu, kwani mimi ninatubia kwa siku mara mia moja".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema katika sijida yake: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe mimi dhambi zangu ndogo zake na kubwa zake za mwanzo wake na mwisho wake, za wazi zake na za siri zake".Imepokelewa Imamu Muslim