Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Qur'an tukufu na Elimu zake

Kutoka kwa Abuu Dardai radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:

Available in 49 languages
«Kutoka kwa Abuu Dardai radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayehifadhi aya kumi za mwanzo wa suratul Kahf, atakingwa na Dajali". Na katika riwaya nyingine: "Za mwisho wa suratul Kahf".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayehifadhi aya kumi kwa moyo wake za mwanzo wa suratul Kahaf atakingwa na kuepushwa na kuhifadhiwa na fitina za Masihi Dajali atakayetoka zama za mwisho na atadai uungu, na fitina zake ni fitina kubwa itakayotokea katika Ardhi tangu kuumbwa kwa Adam mpaka kusimama kwa Kiyama; kwa yale aliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika mambo ya ajabu ambayo atawafitinisha kwayo watakaomfuata, na hii ni kwa sababu mwanzo wa suratul Kahaf kuna maajabu na miujiza mikubwa kuliko fitina na za Dajali kwa watu, atakayezizingatia hatofitinika na Dajali. Na katika riwaya nyingine: Ni aya kumi za mwisho wa sura kuanzia katika kauli yake Mtukufu: "Hivi wanadhani wale waliokufuru kuwa wanaweza kujifanyia..."

Source
Imepokelewa Imamu Muslim
Download image

Saved at original quality