Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Historia na Taarekh.

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:

Available in 49 languages
«Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Hakuwahi kupewa hiyari Mtume rehema na amani ziwe juu yake baina ya mambo mawili hata siku moja isipokuwa atachukua jepesi lake, madamu si dhambi, ikiwa itakuwa ni dhambi, basi hujiwekanalo mbali kuliko watu wote, na hakuwahi kulipiza kisasi Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- katika kitu ambacho kina masilahi yake binafsi katu, isipokuwa kama zitavunjwa sheria za Mwenyezi Mungu, hapo hulipiza kisasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake baadhi ya tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na miongoni mwa zile alizozieleza: Nikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuwahi kupewa hiyari baina ya mambo mawili isipokuwa alichukua jepesi zaidi kati ya hayo, madamu hilo jepesi halipelekei katika madhambi, basi alikuwa akijiweka mbali zaidi kuliko watu wote, na hapo anachagua gumu zaidi. Hakuwahi kulipiza kisasi rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili ya nafsi yake binafsi, bali alikuwa akisamehe na kufuta katika haki yake isipokuwa yakivunjwa maharamisho ya Mwenyezi Mungu hapo analipiza kisasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na alikuwa ni mtu mwenye hasira kuliko watu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality