Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Akida- Itikadi-

Kutoka kwa Muadhi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema:

Available in 71 languages
«Kutoka kwa Muadhi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: Nilikuwa nimepanda Punda nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Punda akiitwa Ufairu, akasema Mtume: "Ewe Muadhi hivi unazijua haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake na zipi haki za waja kwa Mwenyezi Mungu?" Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: " Basi tambua kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni wamuabudu yeye na wala wasimshirikishe na kitu chochote, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu asimwaadhibu yeyote ambaye hajamshirikisha yeye na chochote" Basi nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi kwanini nisiwape watu habari hii? Akasema Mtume: "Usiwape habari hii kwani watabweteka".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anaziweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja ni kuwa wamuabudu yeye peke yake na wala wasimshirikishe yeye na kitu chochote. Na kuwa haki za waja kwa Mwenyezi Mungu ni kutowaadhibu wenye kumpwekesha ambao hawamshirikishi yeye na chochote. Kisha Muadhi akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi kwa nini nisiwape watu habari hii njema ili wafurahi kwa jambo hili bora? Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamkataza kwa kuogopea kuwa watategemea habari hiyo.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality