Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Akida- Itikadi-

Imepokelewa kutoka kwa Jabiri Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema:

Available in 71 languages
«Imepokelewa kutoka kwa Jabiri Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Mtu mmoja alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nini maana ya wawili wenye kustahiki? Akasema: "Yeyote atakaye kufa hali ya kuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi, na atakaye kufa akiwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia motoni"»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Mtu mmoja alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo mawili: ambayo yanasababisha kuingia peponi na yanayo sababisha kuingia motoni? Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akamjibu kuwa mambo ambayo yanamsababishia mtu kupata pepo ni kuwa afe mtu hali yakuwa anamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na wala hamshirikishi na kitu chochote. na kuwa mambo ambayo yanapelekea kuingia motoni, ni kuwa afe mtu hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na anamuwekea Mwenyezi Mungu washirika na vifananishwa katika uungu wake na uumbaji wake na katika majina yake na sifa zake.

Source
Imepokelewa Imamu Muslim
Download image

Saved at original quality