Hadith for the World
Topic

Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

288 hadiths

288 hadiths

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mtu hawi na nguvu kwa kupigana miereka, bali mwenye nguvu ni yule anayeimiliki nafsi yake wakati wa hasira".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: "لِيُسَلِّمِ الصغيرُ على الكبيرِ، والمارُّ على القاعدِ، والقليلُ على الكثيرِ" وفي رواية: "والراكبُ على الماشي".متفق عليه
Kutoka kwa Abuu Masoud Al-Answari -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika kipandwa changu kimeangamia nakuomba msaada wa usafiri, akasema: "Sina uwezo" Mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi nitamuonyesha kwa mtu atakayeweza kumbeba, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayeelekeza katika jambo la kheri basi atapata malipo mfano wa malipo ya mfanyaji wake".Imepokelewa Imamu Muslim
عن علي بن أبي طالب رضي الله عنه مرفوعاً: «إذا انْتَعَل أحدكم فليبدأ باليمين، وإذا نَزَعَ فليبدأ بالشمال، ولْتَكُن اليُمنى أولَهُما تُنْعَل، وآخِرَهُما تُنْزَع».متفق عليه
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Jubairi bin Mutwim -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haingii peponi mkata udugu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema: "Hamtazami Mwenyezi Mungu mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake Amesema: "Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge udugu wake".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «من الكبائر شَتْمُ الرجل والديه» قيل: وهل يسبّ الرجل والديه؟ قال: «نعم، يسبّ أبا الرجل فيسبّ أباه، ويسبّ أمّه، فيسبّ أمّه».متفق عليه
Kutoka kwa Abdul Rahman Bin Abii Laila amesema: Alikutana nami Ka'bu bin Ujza, akasema: Hivi wataka nikupe zaidi? Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema? Akasema: "Basi semeni: Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammadi na juu ya watu wa Muhammadi, kama ulivyompa rehema Ibrahim na juu ya watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa, ewe Mwenyezi Mungu shusha baraka juu ya Muhammad na juu ya watu wa Muhammad, kama ulivyoteremsha baraka kwa watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu,Basi zidisheni dua".Imepokelewa Imamu Muslim
عن أبي أمامة رضي الله عنه قال: سمعتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ: «اقْرَؤُوا القرْآنَ؛ فَإنَّهُ يَأتِي يَوْمَ القِيَامَةِ شَفِيعًا لأَصْحَابِهِ».رواه مسلم
عن أبي ذر الغفاري رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «ألاَ أُخْبِرُكَ بِأَحَبِّ الكَلاَمِ إِلَى اللهِ؟ إنَّ أَحَبَّ الكلام إِلى الله: سبحان اللهِ وبحمدِهِ».رواه مسلم
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze, na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na amkirimu jirani yake, na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na amkirimu mgeni wake".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Asiyewahurumia watu naye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamhurumii"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Neema mbili wamepoteza thamani yake watu wengi: Afya na wakati".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: «والذي نفسي بيده، لو لم تذنبوا، لذهب الله بكم، وجاء بقوم يُذْنِبُونَ، فيستغفرون اللهَ تعالى، فيغفر لهم».رواه مسلم
عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه مرفوعاً: «يُؤْتَى بجهنم يومئذ لها سبعون ألف زِمَامٍ مع كل زمام سبعون ألف ملك يَجُرُّونَهَا».رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema katika sijida yake: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe mimi dhambi zangu ndogo zake na kubwa zake za mwanzo wake na mwisho wake, za wazi zake na za siri zake".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: "Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi kwa wingi, akasema: "Ni uchamungu na tabia njema", na akaulizwa kuhusu mambo yatakayowaingiza watu motoni kwa wingi akasema: "Mdomo na utupu".Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : "الْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ، لَا إلَهَ إلَّا اللَّهُ، وَسُبْحَانَ اللَّهِ، وَاَللَّهُ أَكْبَرُ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إلَّا بِاَللَّهِ".رواه ابن حبان والحاكم، أما النسائي فرواه في الكبرى لكن من حديث أبي هريرة
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala".Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai