Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Akida- Itikadi-

Kutoka kwa Abdillah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema:

Available in 43 languages
«Kutoka kwa Abdillah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakika mmoja wenu anapokufa huonyeshwa makao yake asubuhi na jioni, akiwa katika watu wa peponi basi huonyeshwa katika watu wa peponi, na akiwa katika watu wa motoni basi huonyeshwa katika watu wa motoni, basi husemwa: Haya ndiyo makao yako mpaka atakapokufufua Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba mja anapokufa huonyeshwa mbele yake makao yake na sehemu yake maalumu peponi au motoni, mwanzo wa mchana na mwisho wake; mahali pake peponi, na sehemu yake motoni akiwa ni miongoni mwa watu wa motoni, na huambiwa: Haya ndiyo makao yako utakayofufuliwa kwayo siku ya Kiyama; na katika hilo kuna kuneemeka kwa muumini, na kuadhibiwa kwa kafiri.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality