Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Imesimuliwa kutoka kwa Abdul-Rahman bin Abi Laila, kuwa, siku moja walikuwa kwa Hudhaifa, akaomba maji, Mmajusi mmoja akampa kitu cha kunywa, alipokiweka kikombe mkononi mwake, akakitupa, na akasema: Kwani si nilishamkataza zaidi ya mara moja au mbili - kana kwamba anasema: Sikufanya hivi kwa matashi yangu - bali nilimsikia Mtume, rehema na amani ziwe juu yake akisema:

Available in 60 languages
«Imesimuliwa kutoka kwa Abdul-Rahman bin Abi Laila, kuwa, siku moja walikuwa kwa Hudhaifa, akaomba maji, Mmajusi mmoja akampa kitu cha kunywa, alipokiweka kikombe mkononi mwake, akakitupa, na akasema: Kwani si nilishamkataza zaidi ya mara moja au mbili - kana kwamba anasema: Sikufanya hivi kwa matashi yangu - bali nilimsikia Mtume, rehema na amani ziwe juu yake akisema: “Msivae hariri wala dibaji (Sufi) wala msinywe katika vyombo vya dhahabu au vya fedha, wala msile katika vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu na fedha, kwani ni vyao (Makafiri) katika dunia na sisi ni vyetu Akhera."»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Mtume, Rehema na Amani zimshukie, amekataza wanaume kuvaa hariri za kila aina. Aliwakataza wanaume na wanawake kula na kunywa katika vyombo vya dhahabu na fedha. Akasema kuwa ni kwa ajili ya waumini tu Siku ya Kiyama; Kwa sababu waliviepuka katika ulimwengu huu kwa kumtii Mwenyezi Mungu, Ama makafiri wao si vyao huko akhera. Kwa sababu waliharakisha vizuri vyao katika maisha yao ya dunia kwa kuvitumia, na kuasi kwao amri ya Mwenyezi Mungu.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality