Hadith for the World
Adabu za kisheria.

Adabu za kuvaa.

8 hadiths

8 hadiths

Imesimuliwa kutoka kwa Abdul-Rahman bin Abi Laila, kuwa, siku moja walikuwa kwa Hudhaifa, akaomba maji, Mmajusi mmoja akampa kitu cha kunywa, alipokiweka kikombe mkononi mwake, akakitupa, na akasema: Kwani si nilishamkataza zaidi ya mara moja au mbili - kana kwamba anasema: Sikufanya hivi kwa matashi yangu - bali nilimsikia Mtume, rehema na amani ziwe juu yake akisema: “Msivae hariri wala dibaji (Sufi) wala msinywe katika vyombo vya dhahabu au vya fedha, wala msile katika vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu na fedha, kwani ni vyao (Makafiri) katika dunia na sisi ni vyetu Akhera."Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Omari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayevaa hariri duniani hatoivaa Akhera"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu".Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad
عن علي بن أبي طالب رضي الله عنه مرفوعاً: «إذا انْتَعَل أحدكم فليبدأ باليمين، وإذا نَزَعَ فليبدأ بالشمال، ولْتَكُن اليُمنى أولَهُما تُنْعَل، وآخِرَهُما تُنْزَع».متفق عليه
Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema: "Hamtazami Mwenyezi Mungu mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «بينما رجل يمشي في حُلَّةٍ تُعْجِبُهُ نَفْسُهُ، مُرَجِّلٌ رأسه، يَخْتَالُ في مَشْيَتهِ، إذ خَسَفَ اللهُ به، فهو يَتَجَلْجَلُ في الأرض إلى يوم القيامة".متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Asiangalie mwanaume katika uchi wa mwanaume mwenzie, wala mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie, na wala asijifunike mwanaume na mwanaume mwenzie shuka moja, na wala mwanamke asijifunike na mwanamke mwenzie shuka moja".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Vaeni katika nguo zenu nguo nyeupe, kwani hizo ni katika nguo zenu bora, na wavisheni kwazo maiti wenu".Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ibn Majah