Akida- Itikadi-
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake-:
Available in 55 languages
«Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake-: Yakuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Kiyama, akasema: Lini Kiyama? Akasema: “Umetayarisha nini kwa ajili yake?” Akasema: Hapana, isipokuwa ninampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake. Akasema: “Wewe uko pamoja na unayempenda.” Anas akasema: Hakuna lililotufurahisha zaidi ya kauli ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Wewe uko pamoja na unayempenda.” Anas akasema: Mimi ninampenda Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abubakari na Omari, na ninataraji kuwa pamoja nao kutokana na mapenzi yangu kwao, hata kama nisipofanya sawa na matendo yao.»Meaning translation ·
Saved at original quality








