Hadith for the World
Akida- Itikadi-

Kuamini siku ya mwisho

26 hadiths

26 hadiths

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake-: Yakuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Kiyama, akasema: Lini Kiyama? Akasema: “Umetayarisha nini kwa ajili yake?” Akasema: Hapana, isipokuwa ninampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake. Akasema: “Wewe uko pamoja na unayempenda.” Anas akasema: Hakuna lililotufurahisha zaidi ya kauli ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Wewe uko pamoja na unayempenda.” Anas akasema: Mimi ninampenda Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abubakari na Omari, na ninataraji kuwa pamoja nao kutokana na mapenzi yangu kwao, hata kama nisipofanya sawa na matendo yao.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن مرداس الأسلمي رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ -صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ-: «يذهب الصالحون الأول فالأول، ويبقى حُثَالَةٌ كَحُثَالَةِ الشعير أو التمر لا يُبَالِيهُم الله بَالَةً».رواه البخاري
Kutoka kwa Zainab bint Jahshi radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia ndani kwake akiwa na mfadhaiko huku akisema: “Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ole wao waarabu na watahadhari dhidi ya shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya'juuju na Ma'ajuju upenyo wa kiasi hiki.” Jahshi akasema: Basi nikasema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Je, tuangamie na hali miongoni mwetu wamo watu wema? Akasema: "Ndio, ikiwa maovu yatakithiri".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن معاذ بن أنس رضي الله عنه مرفوعًا: «مَن كَظَمَ غَيظًا، وَهُو قادر على أن يُنفِذَه، دَعَاه الله سبحانه وتعالى على رؤوس الخَلاَئِق يوم القيامة حتَّى يُخَيِّره من الحُور العَين مَا شَاء».رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه وأحمد
عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «إِنَّ الله تَعَالى يَقُول يَوْمَ القِيَامَة: أَيْنَ المُتَحَابُّونَ بِجَلاَلِي؟ اليَوم أُظِلُّهُم فِي ظِلِّي يَوْمَ لاَ ظِلَّ إِلاَّ ظِلِّي».رواه مسلم
Kutoka kwa Ubada bin -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Atakaye shuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mjumbe wake na ni mja wake, nakuwa Issa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na neno lake alilolipeleka kwa Mariam na ni roho toka kwake, na pepo ni kweli na moto ni kweli, atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن معاذ بن جبل رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم أنه قال: «قَالَ اللهُ -عَزَّ وجَلَّ-: المُتَحَابُّون فِي جَلاَلِي، لَهُم مَنَابِرُ مِن نُورٍ يَغْبِطُهُم النَبِيُّونَ والشُهَدَاء».رواه الترمذي وأحمد
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Hakika peponi kuna daraja mia moja kaziandaa Mwenyezi Mungu kwaajili ya wenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kati ya daraja mbili ni kama masafa ya baina ya mbingu na ardhi".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayempa muda mwenye hali ngumu, au akamfutia deni, Allah atampa kivuli siku ya kiyama chini ya kivuli cha Arshi yake siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake."Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Barza Al Aslamia -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hautonyanyuka unyayo wa mja siku ya Kiyama mpaka aulizwe kuhusu umri wake aliumaliza katika mambo yapi? Na kuhusu elimu yake aliifanyia kazi katika nini? Na kuhusu mali yake ni wapi aliichuma? Na aliitoa katika mambo gani? Na kuhusu mwili wake aliumaliza katika mambo yapi?"Imepokelewa Imamu Tirmidhiy
عن أبي أمامة رضي الله عنه قال: سمعتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ: «اقْرَؤُوا القرْآنَ؛ فَإنَّهُ يَأتِي يَوْمَ القِيَامَةِ شَفِيعًا لأَصْحَابِهِ».رواه مسلم
عن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «يُبْعَثُ كلُّ عبدٍ على ما مات عليه».رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Tulikuwa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akautazama mwezi usiku (yaani: Usiku wa tarehe 15) akasema: "Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi huu, hamtokingwa katika kumuona kwake, ikiwa mtaweza kufanya hima msizidiwe mkashindwa kusali kabla ya jua kuchomoza na kabla ya kuzama kwake basi fanyeni hivyo" Kisha akasoma: "Na umtukuze Mola wako kwa himdi zake njema kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Dardai radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayehifadhi aya kumi za mwanzo wa suratul Kahf, atakingwa na Dajali". Na katika riwaya nyingine: "Za mwisho wa suratul Kahf".Imepokelewa Imamu Muslim
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : « سَيْحَانُ وَجَيْحَانُ وَالفُرَاتُ والنِّيل كلٌّ من أنهار الجنة».رواه مسلم
عن أنس بن مالك رضي الله عنه مرفوعاً: «إنَّ الكافر إذا عمل حسنة، أُطْعِمَ بها طُعْمَةً من الدنيا، وأما المؤمن فإِنَّ اللهَ تعالى يدخر له حسناته في الآخرة، ويُعْقِبُهُ رزقًا في الدنيا على طاعته». وفي رواية: «إنَّ الله لا يظلم مؤمنا حسنة، يُعْطَى بها في الدنيا، ويُجْزَى بها في الآخرة، وأما الكافر فَيُطْعَمُ بحسنات ما عمل لله تعالى في الدنيا، حتى إذا أفضى إلى الآخرة، لم يكن له حسنة يُجْزَى بها».رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Waadhini wote watakuwa na shingo ndefu zaidi kuliko watu wote siku ya Kiyama".Imepokelewa Imamu Muslim
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «على أَنْقَابِ المدينةِ ملائكةٌ لا يدخلُها الطَّاعونُ، ولا الدَّجَّالُ».متفق عليه
Na kutoka kwa Jaabir bin Abdillah -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesema wakati anasikia adhana: Allaahumma rabba haadhihid da'watit taamma, was swalaatul qaaima, aati Muhammadanil wasiilata wal fadhwiila, wab'ath-huu maqaaman mahmuudanil ladhii wa a'ttah, (Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa wito huu uliotimia, na swala iliyosimama, mpe Muhammad utetezi na fadhila, na umfufue mahali pakusifiwa ulipomuahidi) basi utakuwa halali kwake utetezi wangu siku ya Kiyama".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Kutoka kwa Abdillah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakika mmoja wenu anapokufa huonyeshwa makao yake asubuhi na jioni, akiwa katika watu wa peponi basi huonyeshwa katika watu wa peponi, na akiwa katika watu wa motoni basi huonyeshwa katika watu wa motoni, basi husemwa: Haya ndiyo makao yako mpaka atakapokufufua Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: "Hakita simama Kiyama mpaka jua lichomoze kutoka upande wa Magharibi, na likichomoza na wakaliona watu wote wataamini, na wakati huo: ((Mtu haitamfaa imani yake ambaye alikuwa hakuamini kabla, au imani yake haikufanya mambo ya kheri:158)) na kwa hakika kitasimama Kiyama na hali yakuwa watu wawili wametandaza nguo zao kwa ajili ya kuuza na kununua na wala hatoweza kuzikunja kutokana na uharaka wa Kiyama, na kwa hakika kitasimama Kiyama ghafla, na kwa hakika ataondoka mtu na maziwa aliyoyachukua kwenye chuchu za mnyama na wala asiwahi kuyanywa, na kitasimama Kiyama wakati anatengeneza josho la kunyweshea na wala asiwahi kunywesheleza, na kwa hakika kitasimama Kiyama na mmmoja wenu atainua tonge kupeleka mdomoni na wala asiweze kula."Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu tu ya sabini itokanayo na moto wa Jahannam" Kukasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ikiwa ni hivyo basi moto wa Duniani unatosha kuadhibu, akasema: "Umeongezewa ukali zaidi yake kwa mara sitini na tisa, na mara zote hizo sitini na tisa kila mara moja ni sawa na ukali wa moto wa duniani."Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
kutoka kwa Abdillah bin Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao- Yakwamba amemsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake anasema: "Mtakapo msikia muadhini basi semeni mfano wa yale anayo yasema, kisha mnitakie rehema, ni kwamba yule atakaye nitakia rehema mara moja Allah atamtakia rehema mara kumi, kisha niombeeni kwa Allah ukaribu, hakika ukaribu huo ni daraja ndani ya Pepo, halipati daraja hilo isipokuwa mja miongoni mwa waja wa Allah, na ninatarajia niwe mimi ndiye huyo mja huyo, na atakayeniombea mimi ukaribu ataupata uombezi".Imepokelewa Imamu Muslim