Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Fiq'hi na misingi yake.

Kutoka kwa Aswadi bin Yadizi amesema:

Available in 41 languages
«Kutoka kwa Aswadi bin Yadizi amesema: Nilimuuliza Aisha, nini alikuwa akifanya Mtume rehema na amani ziwe juu yake nyumbani kwake? Akasema: Alikuwa akishiriki katika kazi za familia yake (anakusudia kuhudumia familia yake), unapofika wakati wa swala anatoka kwenda katika swala.»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Aliulizwa mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kuhusu hali ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake nyumbani kwake, na alikuwa akifanya nini? Akasema: Alikuwa ni mtu kama watu wengine, na anafanya wanayofanya wanaume katika majumba yao, anashughulika na kujihudumia yeye na familia yake; anakamua mbuzi wake mwenyewe, na anashona nguo yake, na anashona kiatu chake, na anatengeneza ndoo yake, na ulikuwa unapofikia wakati wa kusimamishwa swala anatoka kwa ajili yakusali rehema na amani ziwe juu yake bila kuchelewa.

Source
Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Download image

Saved at original quality