Hadith for the World

All hadiths

The complete card collection, filter by chapter

655 hadiths

Kutoka kwa Ummu Dardaai na Abuu Dardaai radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Dua ya mtu muislamu kwa ndugu yake, anapokuwa hayupo, hujibiwa, kichwani kwake huwa kuna Malaika aliyepewa kazi, kila anapomuombea ndugu yake kwa heri, Malaika aliyepewa kazi hiyo husema: Ewe Mwenyezi Mungu pokea dua, na kwako pia upate mfano wake".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Tulikatazwa kusindikiza jeneza, na hatukusisitiziwa katazo hilo.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillah -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u:"Msiziombee mabaya nafsi nakhofia dua hizo zisikutane na muda ambao haombwi Mwenyezi Mungu katika muda huo chochote isipokuwa anakujibuni.Imepokelewa na Imamu Muslim
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- hadithi Marfu'u: "Hujibiwa mmoja wenu anapokuwa hajafanya haraka: anasema: Nimemuomba Mola wangu, na wala sijaona ananijibu mimi" Na katika riwaya ya Muslim: "Hatoacha kuendelea kujibiwa mja madam tu hajaomba dhambi, au kukata ukoo na madam hajafanya haraka" pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kufanya haraka? akasema: "Anasema: Nimeomba, hakika nimeomba, wala sijaona ananijibu, akakata tamaa na wakati huo akaacha kuomba".Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Kutoka kwa Abuu Umama amesema: Alinisimulia Amru bin Abasa radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja ni katikati ya usiku wa mwisho, ikiwa utaweza kuwa miongoni mwa wanaomtaja Mwenyezi Mungu katika wakati huo basi fanya".Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
Kutoka kwa Thauban -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Allah- rehema na amani za Allah ziwe juu yake: "Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na dinari anayoitoa mtu kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari anayoitoa kwa watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu" Amesema Abuu Qilaba: Na ameanza na familia, kisha akasema Abuu Qilaba: Na ni mtu gani mwenye malipo bora kuliko yule anayetoa kwa familia yake wakiwa wadogo, akawazuia na machafu au akawanufaisha Mwenyezi Mungu kupitia hicho na akawatosheleza.Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -sala na amani ziwe juu yake- amesema: "Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni".Imepokelewa Imamu Muslim
عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: «الإيمانُ بِضْعٌ وَسَبْعُونَ أو بِضْعٌ وسِتُّونَ شُعْبَةً: فَأَفْضَلُهَا قَوْلُ: لا إله إلا الله، وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ، وَالحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنَ الإِيمَانِ».متفق عليه
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Pindi mja muislamu au muumini atakapotawadha akaosha uso wake, madhambi yake yote yanayotokana na kuangalia yanaondoka na tone la maji au tone la mwisho usoni mwake, akiosha mikono yake yanaondoka madhambi yote yatokanayo na mikono pamoja na tone la mwisho, akiosha miguu yake madhambi yote yatokanayo na kutembea yanaondoka na tone la mwisho, mpaka muislamu anabaki msafi hana madhambi".Imepokelewa Imamu Muslim
عن معاذ بن أنس رضي الله عنه مرفوعًا: «مَن كَظَمَ غَيظًا، وَهُو قادر على أن يُنفِذَه، دَعَاه الله سبحانه وتعالى على رؤوس الخَلاَئِق يوم القيامة حتَّى يُخَيِّره من الحُور العَين مَا شَاء».رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه وأحمد
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah -radhi za Allah ziwe juu yao (yeye na baba yake), amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitufundisha kutaka uchaguzi (kwa Mwenyezi Mungu) katika mambo yetu yote kama anavyotufundisha sura katika Qur'ani, Akisema: "Atakapo dhamiria mmoja wenu kufanya jambo, basi na aswali rakaa mbili zisizokuwa za faradhi, kisha aseme: 'Allahumma Inniy As-takhiiruka bi ilmika, wa astaq-diruka biqud-ratika wa as-aluka min fadhw-lika al-adhwiim, fa innaka taqdiru walaa aq-diru wata'alamu walaa a'alamu wa anta allaamul ghuyuub, Allahumma inkunta ta'alamu anna haadhal amru- na atataja jambo lenyewe -Khairun lii fii diiniy wadun-yaaya wamaashii wa aaqibatu amriy (Ajiluhuu wa Aajiluhu) Faq-dirhu lii wayassirhuu lii thumma baarik liiy fiihi, wa in kunta ta'alamu anna haadhal amru sharrun lii fii diiniy wa dun yaaya wa maashiy wa Aaqibatu Amriy Fas-rif-huu anniy was-rifniiy anhu waqdir liyal khaira haithu kaana thummar-dhinii bihi" Tafsiri: "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakutaka uchaguzi kupitia elimu yako, na ninakuomba uwezo kupitia uwezo wako, na ninakuomba unipe kutoka katika fadhila zako tukufu, kwani wewe unaweza na mimi siwezi, na unajua na mimi sijui na wewe ni mjuzi wa yaliyofichikana, Ewe Mola wangu ikiwa unajua kuwa jambo hili (Anataja shida yake) ni kheri kwangu katika dini yangu na dunia yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu (iwe kwa haraka au kwa kuchelewa) basi nakuomba niwezeshe na unifanyie wepesi kwangu kisha unibariki mimi ndani ya jambo hili, Na ikiwa unajua kuwa jambo hili ni shari kwangu katika dini yangu na dunia yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu, basi liepushe nami na uniepushe nalo, kisha nipangie heri mahala popote itakapokuwa kisha niridhishe nayo".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: مرَّ النَّبي - صلى الله عليه وسلم - بامرَأَة تَبكِي عِند قَبرٍ، فقال: «اتَّقِي الله واصْبِري» فقالت: إليك عَنِّي؛ فَإِنَّك لم تُصَب بِمُصِيبَتِي ولم تَعرِفه، فقِيل لها: إِنَّه النَّبِي - صلى الله عليه وسلم - فأتت باب النبي - صلى الله عليه وسلم - فلم تجد عنده بوَّابِين، فقالت: لم أَعرِفكَ، فقال: «إِنَّما الصَّبرُ عِند الصَّدمَةِ الأُولَى». وفي رواية: «تَبكِي على صبِّي لها».متفق عليه
Kutoka kwa Suhaib -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Ajabu iliyoje ya jambo la muumini, hakika jambo lake lote ni kheri, na hakuna hilo kwa yeyote ila kwa muumini, akipatwa na jambo lenye kufurahisha anashukuru ikawa hilo ni kheri kwake, na akipatwa na madhara anasubiri likawa hilo ni kheri kwake."Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Yalikuwa maneno ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni maneno ya wazi anayaelewa kila mwenye kuyasikia.Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na An-Nasaaiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad
عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه مرفوعاً: «إِنَّ مِنْ أَشَرِّ النَّاسِ عِندَ الله مَنزِلَةً يَومَ القِيَامَةِ الرَّجُلَ يُفضِي إِلَى المَرْأَةِ وَتُفْضِي إِلَيه، ثُمَّ يَنشُرُ سِرَّهَا».رواه مسلم
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yapi hayo? Akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na uchawi, na kuua nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki, na kula riba, na kula mali ya yatima, na kukimbia siku ya vita, na kuwatuhumu machafu waumini wa kike waliojihifadhi wasiojua lolote (kuhusu huo uchafu)"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu, Allah amewalaani watu walioyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa misikiti".Imepokelewa na Ahmad
Kutoka kwa Anas bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na Amani zimfikie, yakuwa yeye Amesema: "Hakika ukubwa wa malipo huendana sawa pamoja na ukubwa wa matatizo, na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapowapenda watu huwapa mtihani; atakayeridhia atapata radhi, na atakayechukia atapata hasira (za Mwenyezi Mungu)."Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Amesema Allah aliyetakasika na kutukuka: Mimi nimetosheka (sihitaji) washirika kushirikishwa nao, yeyote mwenye kufanya jambo akashirikisha ndani yake mwingine pamoja nami, nitamuacha na ushirika wake".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Ally -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "Waelezeni watu yale wanayoyafahamu, Hivi mnataka akadhibishwe (apingwe) Mwenyezi Mungu na Mtume wake?".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, na nitakieni rehema, kwani dua zenu hunifikia mahala popote muwapo".Imepokelewa na Abu Daud
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -sala na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu hupata wivu, na hakika muumini hupata wivu, na wivu wa Mwenyezi Mungu ni pale muumini anapoyafanya yale aliyomharamishia juu yake".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu".Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Atakaye walea mabinti wawili mpaka wakafikia utu uzima atakuja siku ya Kiyama mimi na yeye (Namna hii)" Na akaviunganisha vidole vyake viwili.Imepokelewa Imamu Muslim