Hadith for the World
Fiq'hi ya Tabia.

Tabia njema.

35 hadiths

35 hadiths

Imepokewa kutoka kwa Sa'd bin Abii Waqas -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika Mwenyezi Mungu humpenda mja mchamungu, mwenye kutosheka, mnyenyekevu".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini iliyekamilika zaidi imani yake ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine, na mbora wenu ni yule mbora wenu kwa wake zake".Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe kwake- mke wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anasimulia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alisema: "Hakika upole hauwi ndani ya kitu isipokuwa hukipendezesha, na hautolewi ndani ya kitu ila hukichafua".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika muumini hufikia kwa sababu ya tabia zake njema daraja ya mfungaji mwenye kusimama usiku".Imepokelewa na Abu Daud na Ahmad
Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hakuwa na maneo machafu wala mwenye kuyatafuta, na alikuwa akisema: "Hakika katika wabora wenu ni mtu mwenye tabia njema kuliko wote".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fanyeni mambo kuwa mepesi na wala msiyafanye kuwa magumu, na wapeni watu bishara njema na wala msiwakimbize".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mlisheni mwenye njaa, na mtembeleeni mgonjwa, na mwacheni huru mateka".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Imepokewa Kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Wenye huruma huwahurumia Ar-Rahmani -Mwingi wa huruma-, wahurumieni walioko ardhini atakuhurumieni aliyeko mbinguni."Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
Imepokelewa kutoka kwa Abdillah Bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Muislamu wa kweli ni yule wanayepata Amani waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake, na mhamaji ni yule mwenye kuyahama yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عَن أَبي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَامَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي صَلاَةٍ وَقُمْنَا مَعَهُ، فَقَالَ أَعْرَابِيٌّ وَهُوَ فِي الصَّلاَةِ: اللَّهُمَّ ارْحَمْنِي وَمُحَمَّدًا، وَلاَ تَرْحَمْ مَعَنَا أَحَدًا. فَلَمَّا سَلَّمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ لِلْأَعْرَابِيِّ: «لَقَدْ حَجَّرْتَ وَاسِعًا» يُرِيدُ رَحْمَةَ اللهِ.رواه البخاري
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِنَّ اللَّهَ قَالَ: إِذَا ابْتَلَيْتُ عَبْدِي بِحَبِيبَتَيْهِ فَصَبَرَ، عَوَّضْتُهُ مِنْهُمَا الجَنَّةَ» يُرِيدُ: عَيْنَيْهِ.رواه البخاري