Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Fiq'hi na misingi yake.

Kutoka kwa Abuu Zuhairi Umara bin Ruaiba radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:

Available in 54 languages
«Kutoka kwa Abuu Zuhairi Umara bin Ruaiba radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kamwe, hatoingia motoni mtu yeyote aliyeswali kabla ya kuchomoza Jua na kabla ya kuzama kwake"»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa hatoingia motoni mtu yeyote aliyeswali swala ya Alfajiri, na swala ya Lasiri, na akadumu nazo; na amezitaja maalumu swala hizi mbili; kwa sababu ndizo swala nzito zaidi, na kwa sababu wakati wa Alfajiri huwa ni wakati wa usingizi na ladha yake, na wakati wa Lasiri huwa ni wakati wa kushughulishwa na kazi za mchana na biashara zake, na atakayezihifadhi swala hizi mbili pamoja na kupatikana tabu ndani yake, basi bila shaka ataweza kuzihifadhi swala zingine zilizobakia.

Source
Imepokelewa Imamu Muslim
Download image

Saved at original quality