Hadith for the World

All hadiths

The complete card collection, filter by chapter

655 hadiths

عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه مرفوعاً: «يُؤْتَى بجهنم يومئذ لها سبعون ألف زِمَامٍ مع كل زمام سبعون ألف ملك يَجُرُّونَهَا».رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema katika sijida yake: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe mimi dhambi zangu ndogo zake na kubwa zake za mwanzo wake na mwisho wake, za wazi zake na za siri zake".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: "Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi kwa wingi, akasema: "Ni uchamungu na tabia njema", na akaulizwa kuhusu mambo yatakayowaingiza watu motoni kwa wingi akasema: "Mdomo na utupu".Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : "الْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ، لَا إلَهَ إلَّا اللَّهُ، وَسُبْحَانَ اللَّهِ، وَاَللَّهُ أَكْبَرُ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إلَّا بِاَللَّهِ".رواه ابن حبان والحاكم، أما النسائي فرواه في الكبرى لكن من حديث أبي هريرة
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala".Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu, na unitengenezee dunia yangu ambayo kunapatikana maisha yangu, na unitengenezee Akhera yangu ambako kunapatikana kuishi kwangu milele, na unijalie ziada ya uhai kwenye kila lenye heri, na ujalie kifo ni kitulizo changu kutokana na kila shari"Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Abuu Mussa radhi za Allah ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba yeye alikuwa akiomba kwa dua hii: "Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote, na yale unayoyajua kutoka kwangu, ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu, na yale ya makusudi na ujinga wangu na mzaha wangu, na hayo yote yaliyo kwangu, ewe Mola wangu nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza, wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji, na wewe juu ya kila kitu ni muweza".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiacha dua hizi, kila anaposhinda jioni na kila anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba msamaha na afya katika dini yangu na dunia yangu na familia yangu na mali yangu, ewe Mwenyezi Mungu sitiri uchi wangu -Au aibu zangu- na utie amani yote ninayoyahofia, ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi toka mbele yangu, na nyuma yangu, na kuliani kwangu, na kushotoni kwangu, na juu yangu, na ninajilinda kwa utukufu wako nisijekuvamiwa tokea chini yangu".Imepokelewa na Abu Daud, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
kutoka kwa Abdullahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Ilikuwa miongoni mwa dua za Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa afya yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na kila aina ya hasira zako"Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Abdillah bin Amry bin Aaswi radhi za Allah ziwe juu yao wote wawili yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiomba kwa maneno haya: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui"Imepokelewa na Nasai na Ahmad
عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «المؤمن الذي يخالط الناس، ويصبر على أذاهم خير من الذي لا يخالط الناس ولا يصبر على أذاهم».رواه الترمذي وابن ماجه وأحمد
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri, Pupia yenye manufaa na wewe, na utake msaada kwa Allah na wala usishindwe, na likikusibu jambo usiseme: Lau ningelifanya kadha basi ingelikuwa kadhaa wa kadhaa, lakini sema: Hili ni kwa makadirio ya Allah naye hufanya alitakalo, maana neno "Lau" hufungua matendo ya shetani".Imepokelewa Imamu Muslim
عن أبي هريرة رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «الْمُؤْمِنُ مِرْآةُ أَخِيهِ الْمُؤْمِنِ».رواه أبو داود والترمذي
Imepokelewa kutoka kwa Abud-dardaa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi siku ya Kiyama".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokewa Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Dua ndio ibada", Kisha akasoma: "Na amesema Mola wenu Mlezi niombeni mimi nitakujibuni, hakika wale wanaofanya kiburi katika ibada yangu wataingia Jahannam wakiwa madhalili" [Ghafir: 60].Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Kutoka kwa Iyaadh bin Himari ndugu yao na Bani Mujashii radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alisimama kwetu Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake siku moja kwa ajili ya kuhutubia, akasema: Na akaeileza hadithi na ndani yake alisema: "Na hakika Mwenyezi Mungu ameniteremshia wahyi kuwa, kuweni wanyenyevu, mpaka asijikweze yeyote kwa mwingine, na wala asimfanyie uadui yeyote mwenzake"Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mazuri, na Akhera mazuri, na utukinge na adhabu ya moto".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Shadaad Bin Ausi Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Bwana wa Istighfari (Dua ya kuomba msamaha) Ni kusema: Allaahumma anta Rabbi Laa ilaaha illaa anta, khalaqtani wa anaa abduka wa ana a'laa a'hdika, wawa'dika mastatwa'tu, auudhubika min Sharri maa swana'tu, abuu ulaka bini'matika alaiyya, wa abuu ulaka bidhambi faghfirlii, fa innahuu laa yaghfirudh-dhunuuba illaa anta" Akasema: "Na atakayeisema dua hii mchana akiwa na yakini nayo, akafa katika mchana wake huo kabla hajafika jioni, basi atakuwa miongoni mwa watu wa peponi, na atakayeisema wakati wa usiku akiwa na yakini nayo, akafariki kabla hajafika asubuhi, basi huyo atakuwa miongoni mwa watu peponi".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: Kutoka kwa Abdillah bin Mas'udi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Shikamaneni na ukweli, kwani ukweli hupelekea katika wema, na hakika wema hupelekea katika pepo, na hatoacha mtu kuwa mkweli na akishughulika na ukweli mpaka ataandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli, na tahadharini na uongo, kwani uongo unapelekea katika uovu, na hakika uovu hupelekea katika moto, na hatoacha mtu kuendelea kuwa muongo, na akishughulika na uongo mpaka ataandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni muongo".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Maneno mawili mepesi mno katika ulimi, ni mazito mno katika mizani, yanapendeka mno kwa Al-Rahmani (Mwingi wa rehema) Ni: Sub-haanallahil Adhwiim, Sub-haanallaahi wabihamdihi".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna kitu kinachotukuzwa zaidi kwa Allah Mtukufu kuliko dua".Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Sadaka haikuwahi kupunguza chochote katika mali, na hakuna jambo zuri zaidi analomzidishia Mwenyezi Mungu mja kwa kusamehe zaidi kama kupewa utukufu, na hakuwahi kunyenyekea yeyote kwa ajili Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu humnyanyua".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokewa kutoka kwa Abuu Dardaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeitetea heshima ya ndugu yake basi Mwenyezi Mungu ataukinga uso wake na moto siku ya Kiyama".Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad