Hadith for the World
Topic

Akida- Itikadi-

135 hadiths

135 hadiths

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Barza Al Aslamia -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hautonyanyuka unyayo wa mja siku ya Kiyama mpaka aulizwe kuhusu umri wake aliumaliza katika mambo yapi? Na kuhusu elimu yake aliifanyia kazi katika nini? Na kuhusu mali yake ni wapi aliichuma? Na aliitoa katika mambo gani? Na kuhusu mwili wake aliumaliza katika mambo yapi?"Imepokelewa Imamu Tirmidhiy
عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: «لما خلق اللهُ الخَلْقَ كتب في كتاب، فهو عنده فوق العرش: إن رحمتي تَغْلِبُ غضبي». وفي رواية: «غَلَبَتْ غضبي» وفي رواية: «سَبَقَتْ غضبي».متفق عليه
kutoka kwa Nu'man Bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake -: "Mfano wa waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao na kufanyiana kwao upole, ni kama mfano wa kiwiliwili, kinapopata tabu kiungo kimoja vinaitana kwa ajili ya hicho kimoja viungo vyote kwa kukesha na maumivu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ni dhambi ipi kubwa zaidi mbele ya Allah? Akasema: "Ni wewe kumuwekea Mwenyezi Mungu mshirika, na hali yeye ndiye aliyekuumba" Nikasema: Hakika hilo ni jambo kubwa, nikasema: Kisha ipi? Akasema: "Na kumuua mwanao; ukiogopea atakula pamoja nawe" Nikasema: Kisha ipi? Akasema: "Ni wewe kumzini mke wa jirani yako".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
kutoka kwa Abuu Swirma -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakayewatia watu ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtilia ugumu".Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Masudi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Si miongoni mwetu atakayepiga mashavu, na akachana mifuko, na akaomboleza kwa maombolezo ya watu wa zama za ujinga".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي أمامة رضي الله عنه قال: سمعتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ: «اقْرَؤُوا القرْآنَ؛ فَإنَّهُ يَأتِي يَوْمَ القِيَامَةِ شَفِيعًا لأَصْحَابِهِ».رواه مسلم
عن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «يُبْعَثُ كلُّ عبدٍ على ما مات عليه».رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri, Pupia yenye manufaa na wewe, na utake msaada kwa Allah na wala usishindwe, na likikusibu jambo usiseme: Lau ningelifanya kadha basi ingelikuwa kadhaa wa kadhaa, lakini sema: Hili ni kwa makadirio ya Allah naye hufanya alitakalo, maana neno "Lau" hufungua matendo ya shetani".Imepokelewa Imamu Muslim
عن أنس بن مالك رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم أنه كان إذا أكل طعاما، لعق أصابعه الثلاث. قال: وقال: «إذا سقطت لُقمة أحدكم فليُمِطْ عنها الأذى، وليأكلها ولا يَدَعْهَا للشيطان» وأمر أن تُسْلَتَ القَصْعَةُ، قال: «فإنكم لا تدرون في أيِّ طعامكم البركة» وعن جابر بن عبد الله رضي الله عنه أن رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قالَ: "إنّ الشيطانَ يَحضُرُ أحدَكُم عندَ كلِ شيءٍ من شَأنِه، حتى يَحضُرَهُ عندَ طعامِهِ، فإذا سَقطتْ لقمةُ أحدِكُم فليَأخُذْها فَلْيُمِطْ ما كانِ بها من أذى، ثم ليَأكُلْها ولا يَدَعْها للشيطانِ، فإذا فَرَغَ فليَلْعَقْ أصابعَهُ، فإنه لا يَدري في أيِّ طَعامه البركة"حديث أنس رواه مسلم. حديث جابر رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Tulikuwa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akautazama mwezi usiku (yaani: Usiku wa tarehe 15) akasema: "Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi huu, hamtokingwa katika kumuona kwake, ikiwa mtaweza kufanya hima msizidiwe mkashindwa kusali kabla ya jua kuchomoza na kabla ya kuzama kwake basi fanyeni hivyo" Kisha akasoma: "Na umtukuze Mola wako kwa himdi zake njema kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Musa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu humpa muda dhalimu, mpaka akija kumuadhibu hambakishi" Anasema: Kisha akasoma: "Na hivyo ndivyo kuadhibu kwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali" [Hud:102]Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa baadhi ya wake za Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayemuendea mpiga ramli akamuuliza kuhusu lolote hazitokubaliwa sala zake siku arobaini".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Abdillahi bin Masoud Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake yakwamba yeye amesema: "Madhambi makubwa kuliko yote: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kujiaminisha na vitimbi vya Mwenyezi Mungu, na kukata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu, Na kufa moyo katika huruma za Mwenyezi Mungu".Imepokelewa na Abdul Razaaq
عن البراء بن عازب –رضي الله عنهما- قال: كانَ رجلٌ يَقرَأُ سُورةَ الكهفِ، وعندَه فَرَسٌ مَربُوطٌ بِشَطَنَيْنِ، فَتَغَشَّتْهُ سَحَابَةٌ فَجَعَلَتْ تَدْنُو، وجَعلَ فَرَسُه يَنفِرُ منها، فلمّا أصبحَ أتَى النبيَّ صلى الله عليه وسلم فَذَكرَ ذلك له، فقالَ: «تِلكَ السَّكِينةُ تَنَزَّلَتْ للقُرآنِ».متفق عليه
Kutoka kwa Abuu Dardai radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayehifadhi aya kumi za mwanzo wa suratul Kahf, atakingwa na Dajali". Na katika riwaya nyingine: "Za mwisho wa suratul Kahf".Imepokelewa Imamu Muslim
عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «ما توطَّنَ رجلٌ مسلمٌ المساجدَ للصلاة والذِّكر، إلا تَبَشْبَشَ اللهُ له، كما يَتَبَشْبَشُ أهلُ الغائب بغائبهم إذا قَدِمَ عليهم».رواه ابن ماجه وأحمد
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu amesema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja kwa kitu ninachokipenda katika vile nilivyomfaradhishia juu yake, na akawa bado mja wangu anaendelea kujiweka karibu yangu kwa ibada za sunna (zisizokuwa za lazima) mpaka nitafikia mahala nitampenda, nikishampenda: Nitakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analotazamia, na mkono wake anaoshikia, na mguu wake anaotembelea, na hata akiniomba hakika nitampa, na hata akinitaka kinga hakika nitamlinda, na sijawahi kusita katika jambo lolote ninalotaka kulifanya kama kusita kwangu katika (kuitoa) nafsi ya muumini, hapendi kufa na mimi sipendi kumuudhi".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
عن أنس بن مالك وأبي هريرة رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم فيما يرويه عن ربه عز وجل قال: «إذا تَقَرَّبَ العبدُ إليَّ شِبْرًا تَقَرَّبْتُ إليه ذِرَاعًا، وإذا تَقَرَّبَ إليَّ ذِرَاعًا تَقَرَّبْتُ مِنْهُ بَاعًا، وإذا أتاني يمشي أَتَيْتُهُ هَرْوَلَةً».حديث أنس -رضي الله عنه- رواه البخاري . حديث أبي هريرة -رضي الله عنه- متفق عليه
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Imani ni zaidi ya vitengo sabini au zaidi ya sitini, bora yake ni kauli ya Laa ilaaha illa llaah, na ya chini yake ni kuondoa udhia barabarani, na haya ni sehemu katika imani".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Ka'bu bin Hatim -radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ataongeleshwa na Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama bila ya kuwapo na mkalimani yeyote kati yake na Yeye (Allah). Atatazama kuliani kwake, na wala hataona kitu chochote isipokuwa matendo yake aliyotanguliza. Kisha ataangalia kushotoni kwake, na wala hataona kitu chochote isipokuwa matendo yake aliyotanguliza. Na ataangalia mbele yake, na hataona isipokuwa Moto mbele ya uso wake. Basi uepukeni Moto hata kama ni kwa nusu ya tende."Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abdillah bin Hakim- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho".Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Ahmad
Kutoka kwa Twariki bin Ashiyam Al-Ashjai Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayesema: Laa ilaah illa llaah, na akayapinga yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu itakuwa haramu mali yake na damu yake, na hesabu yake itakuwa juu ya Allah".Imepokelewa Imamu Muslim