64 hadiths
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayemtatulia muumini tatizo moja katika matatizo ya dunia, Mwenyezi Mungu atamtatulia yeye tatizo katika matatizo ya siku ya Kiyama, na atakayemfanyia wepesi mwenye ugumu (katika jambo lake) Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi duniani na Akhera, na atakayemsitiri muislamu Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera, na Mwenyezi Mungu humsaidia mja pale mja anapokuwa katika kumsaidia ndugu yake, na atakayeshika njia akitafuta ndani yake elimu, Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi kupitia njia hiyo njia ya kuingia peponi, na hawajawahi kukusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu wakisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na wakisomeshana baina yao, isipokuwa huwashukia utulivu na huwagubika rehema na Malaika huwafunika, na Mwenyezi Mungu huwataja (vizuri) kwa wale walioko kwake (Malaika), na yeyote ambaye matendo yake yatamchelewesha kuingia peponi basi ukoo wake hautompeleka mbio (kuingia)".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, katika yale anayoyasimulia kutoka kwa Mola wake Mtukufu, amesema: "Mja alifanya dhambi akasema: Ee Mola wangu nisamehe dhambi yangu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, na humsitiri kwa ndambi hiyo au humuadhibu kwa kutenda dhambi, kisha akarudi tena akatenda dhambi, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe dhambi yangu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, na ana adhibu kwa kutenda dhambi, fanya utakavyo nimekusamehe".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abdullah bin Salam radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alipokuja Madina Mtume rehema na amani ziwe juu yake, watu walikusanyika mbele yake, pakasemwa: Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu, Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu, wakasema mara tatu, nikaja pamoja na watu kutazama, na nilipouona uso wake nikajua kuwa uso wake si uso wa muongo, kwa hivyo jambo la kwanza nililomsikia akizungumza alisema kuwa: "Enyi watu, toleaneni salamu na muunge udugu, na mlishe chakula, na msali usiku watu wakiwa wamelala, mtaingia peponi kwa amani".Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad