Hadith for the World
Topic

Akida- Itikadi-

135 hadiths

135 hadiths

عن أبي موسى رضي الله عنه قال: سَمَّى لنا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم نفْسَه أسْماءً منها ما حَفِظْنا فقال: «أنا محمد، وأحمد، والمُقَفِّي، والحاشِر، ونبي الرَّحمة، قال يزيد: ونبِيُّ التوبة ونَبِيُّ المَلْحَمة».رواه مسلم وأحمد
عن أنس بن مالك رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم رأى نُخْامَة في القِبْلَة، فَشَقَّ ذلك عليه حتى رُئِي في وجْهِه، فقام فَحَكَّه بِيَده، فقال: «إن أحدكم إذا قام في صلاته فإنه يُنَاجِي رَبَّه، أو إن رَبَّه بينه وبين القِبْلَة، فلا يَبْزُقَنَّ أحدُكم قِبَل قِبْلتِه، ولكن عن يَسَاره أو تحت قَدَمَيه» ثم أخذ طَرف رِدَائِه، فَبَصَقَ فيه ثم ردَّ بَعْضَهُ على بعض، فقال: «أو يفعل هكذا».متفق عليه
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mama Salama alimsimulia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kisa cha kanisa aliloliona katika ardhi ya Ethiopia, likiitwa kanisa la Mtakatifu Maria, akasimulia aliyoyaona ndani yake miongoni mwa picha, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Watu hao anapokufa kwao mja mwema, au mwanaume mwema, wanajenga juu ya kaburi lake mahala pakuabudia, na wanachora ndani yake picha hizo, hao ndio viumbe waovu zaidi mbele ya AllahWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwatukane Maswahaba wangu, kwa sababu, lau kama yeyote kati yenu atatoa dhahabu sawa na (mlima) Uhud (katika njia ya Mwenyezi Mungu), basi haiwezi kuwa sawa na theluthi mbili ya kilo ya mmoja wao wala nusu yake."Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن المسور بن مخرمة رضي الله عنهما مرفوعًا: «فاطمة بَضْعة مني، فمَن أغضبها أغضبني».متفق عليه
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم : «مَن أحبَّ الحسن والحُسين فقد أحبَّني، ومَن أبغضهما فقد أبغضني».رواه ابن ماجه وأحمد
عن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «خيرُكم خيركم لأهلي مِن بعدي». قال: فباع عبد الرحمن بن عوف حديقةً بأربع مائة ألف، فقسَّمها في أزواج النبي صلى الله عليه وسلم .رواه ابن أبي عاصم والحاكم
عن أبي موسى رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «كَمُل من الرجال كثير، ولم يَكمُل من النساء: إلا آسية امرأة فرعون، ومريم بنت عِمران، وإنَّ فضلَ عائشة على النساء كفضل الثَّرِيد على سائر الطعام».متفق عليه
عن عبد الرحمن بن أبي عميرة وكان من أصحاب رسول الله صلى الله عليه وسلم عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال لمعاوية: «اللهم اجعله هاديًا مَهْديًّا واهدِ به».رواه الترمذي وأحمد
عن أبي عزة الهذلي رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله وسلم: «إذا أراد اللهُ قَبْضَ عبد بأرض جعلَ له بها حاجة».رواه الترمذي وأحمد وأبو داود الطيالسي
Kutoka kwa Abdillah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakika mmoja wenu anapokufa huonyeshwa makao yake asubuhi na jioni, akiwa katika watu wa peponi basi huonyeshwa katika watu wa peponi, na akiwa katika watu wa motoni basi huonyeshwa katika watu wa motoni, basi husemwa: Haya ndiyo makao yako mpaka atakapokufufua Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أسامة بن زيد رضي الله عنهما قال: أشرفَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم على أُطُم من آطام المدينة، فقال: «هل ترون ما أرى؟» قالوا: لا، قال: «فإنِّي لأرى الفتنَ تقع خِلال بيوتكم كوَقْع القَطْر».متفق عليه
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «إن لله تِسْعَةً، وتِسْعِينَ، اسْمًا، مِائَةً إلا واحدا مَنْ أَحْصَاهَا دخل الجنة».متفق عليه
kutoka kwa Abdullahi bin Amry -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Umejengwa uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mja wake na Mtume wake, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba tukufu, na kufunga ramadhani".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Hadithi imepokelewa na Abii Said Alkhuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Yeyote miongoni mwenu atayeona jambo ovu na baya basi aliondoshe kwa mkono wake, ikiwa hawezi kuliondoa kwa mkono wake basi aliondoe kwa ulimi wake, na ikiwa hawezi kuliondoa kwa ulimi basi na alichukie kutoka moyoni mwake, na kuchukia moyoni ni udhaifu wa imani".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelea kutoka kwa Abii Maalik Al-Ash-ariy Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake: "Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi na Swala ni nuru, na sadaka ni dalili ya imani, na subira ni mwangaza, na Qur'ani ni hoja kwako au hoja dhidi yako, watu wote huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kutafuta riziki kuna mwenye kuwa na msimamo na kumtii Mwenyezi Mungu, na akawa ni mwenye kuikomboa nafsi yake kutoingia motoni, na miongoni mwao kuna mwenye kuangukia kwenye maasi na akaangamia na kuingia motoni".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Muadhi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: Nilikuwa nimepanda Punda nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Punda akiitwa Ufairu, akasema Mtume: "Ewe Muadhi hivi unazijua haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake na zipi haki za waja kwa Mwenyezi Mungu?" Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: " Basi tambua kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni wamuabudu yeye na wala wasimshirikishe na kitu chochote, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu asimwaadhibu yeyote ambaye hajamshirikisha yeye na chochote" Basi nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi kwanini nisiwape watu habari hii? Akasema Mtume: "Usiwape habari hii kwani watabweteka".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Mtu mmoja alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nini maana ya wawili wenye kustahiki? Akasema: "Yeyote atakaye kufa hali ya kuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi, na atakaye kufa akiwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia motoni"Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, bin Jud'aan kabla ya uislamu alikuwa akiunga udugu, na akilisha masikini, je hilo litamfaa?Akasema: "Halitamnufaisha, na hakika yeye hajawahi kusema hata siku moja: Ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu siku ya Kiyama."Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Sufiani bin Abdillah Al-Thaqafi Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Nieleze ndani ya Uislamu kauli ambayo sitomuuliza yeyote zaidi yako, akasema: "Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo".Imepokelewa na Muslim na Ahmad
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: "Hakita simama Kiyama mpaka jua lichomoze kutoka upande wa Magharibi, na likichomoza na wakaliona watu wote wataamini, na wakati huo: ((Mtu haitamfaa imani yake ambaye alikuwa hakuamini kabla, au imani yake haikufanya mambo ya kheri:158)) na kwa hakika kitasimama Kiyama na hali yakuwa watu wawili wametandaza nguo zao kwa ajili ya kuuza na kununua na wala hatoweza kuzikunja kutokana na uharaka wa Kiyama, na kwa hakika kitasimama Kiyama ghafla, na kwa hakika ataondoka mtu na maziwa aliyoyachukua kwenye chuchu za mnyama na wala asiwahi kuyanywa, na kitasimama Kiyama wakati anatengeneza josho la kunyweshea na wala asiwahi kunywesheleza, na kwa hakika kitasimama Kiyama na mmmoja wenu atainua tonge kupeleka mdomoni na wala asiweze kula."Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu tu ya sabini itokanayo na moto wa Jahannam" Kukasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ikiwa ni hivyo basi moto wa Duniani unatosha kuadhibu, akasema: "Umeongezewa ukali zaidi yake kwa mara sitini na tisa, na mara zote hizo sitini na tisa kila mara moja ni sawa na ukali wa moto wa duniani."Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Amrou Bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Aliandika Mwenyezi Mungu makadirio ya viumbe kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, akasema: Na Arshi yake ilikuwa juu ya maji."Imepokelewa Imamu Muslim
kutoka kwa Abdillah bin Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao- Yakwamba amemsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake anasema: "Mtakapo msikia muadhini basi semeni mfano wa yale anayo yasema, kisha mnitakie rehema, ni kwamba yule atakaye nitakia rehema mara moja Allah atamtakia rehema mara kumi, kisha niombeeni kwa Allah ukaribu, hakika ukaribu huo ni daraja ndani ya Pepo, halipati daraja hilo isipokuwa mja miongoni mwa waja wa Allah, na ninatarajia niwe mimi ndiye huyo mja huyo, na atakayeniombea mimi ukaribu ataupata uombezi".Imepokelewa Imamu Muslim