Hadith for the World

All hadiths

The complete card collection, filter by chapter

655 hadiths

عن ابن مسعود رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «أيُّكم مالُ وارثِه أحَبُّ إليه من مالَه؟» قالوا: يا رسول الله، ما منَّا أحد إلا مَالُه أحَبُّ إليه. قال: «فإن مالَه ما قدَّم، ومالُ وارثِه ما أخَّر».رواه البخاري
Imepokelewa Kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fikisheni kutoka kwangu japokuwa aya moja, na simulieni kuhusu wana wa Israeli wala hakuna ubaya, na yeyote atakayenisemea uongo mimi kwa makusudi basi na ajiandae, makazi yake ni motoni".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba mtu wa kijijini alimjia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akasema: Nijulishe juu ya amali ambayo nikiifanya nitaingia peponi. Akasema: "Umuabudu Mwenyezi Mungu na wala usimshirikishe na chochote, na usimamishe swala na utoe zaka ya wajibu, na ufunge mwezi wa ramadhani" Akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, sitozidisha zaidi ya hapo, basi alipoondoka, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayependezwa na kumtazama mtu miongoni mwa watu wa peponi basi na amtazame huyu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Sahli bin Sa'di Assaaidiy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Laiti Dunia ingelingana na ubawa wa mbu kwa thamani yake mbele ya Allah mtukufu basi kafiri asingekunywa fundo moja la maji".Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy
Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haumpati muislamu uchovu wala maradhi, wala msongo, wala huzuni, wala udhia, wala shida, hata mwiba unaomchoma, isipokuwa anamfutia Mwenyezi Mungu kupitia hilo makosa yake."Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni tano: Kujibu salamu, na kumtembelea mgonjwa, na kufuata jeneza, na kuitika wito, na kumuombea dua mwenye kupiga chafya".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي مسعود البدري رضي الله عنه قَال: قَالَ رَسُولُ اللَّه -صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم-: «حُوسِب رجُل ممن كان قَبْلَكُمْ، فلم يُوجد له من الخَيْر شيء، إلا أنه كان يُخَالط الناس وكان مُوسِراً، وكان يأمُر غِلْمَانَه أن يَتَجَاوَزُوا عن المُعْسِر، قال الله عز وجل : نحن أحَقُّ بذلك منه؛ تَجَاوزُوا عنه».رواه مسلم
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: “Siku bora zaidi iliyochomozewa jua ni siku ya Ijumaa, ndani yake aliumbwa Adam, na ndani yake aliingizwa Peponi, na ndani ya siku hii akatolewa humo, na hakitosimama Kiyama ila siku ya Ijumaa".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika milango, lau angeliapia kwa Mwenyezi Mungu angelimuepusha".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Allah amhurumie mtu ambaye ni mpole anapouza, na anaponunua, na anapo dai deni".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), atakayewakuta wazazi wake wawili wakati wa utuuzima, mmoja wao au wote wawili, na akawa hakuingia peponi".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akitembea katika njia ya kuelekea Makka, akapita karibu na mlima Jumdan, akasema: “Tembeeni huu ni mlima Jumdan, Wamepata ushindi wenye kujitenga” Wakasema: Ni akina nani hao wenye kujitenga ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Ni wenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi katika Wanaume, na wenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi katika wanawake.”Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Ma'adan Bin Abi Twalha Alya'mary amesema: Nilikutana na Thauban muachwa huru wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikasema: 'Niambie matendo nitakayo yafanya (iwe sababu kwa Allah) kuniingiza Peponi' au alisema, nikasema: matendo mazuri yanayopendeka zaidi kwa Allah, akanyamaza, kisha nikamuuliza akanyamaza, kisha nikamuuliza kwa mara ya tatu akasema: Nilimuuliza hayo Mtume wa Allah rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Shikamana na kusujudu kwa wingi kwa ajili ya Allah, kwani hakika wewe huta sujudu kwa ajili ya Allah isipokuwa Allah atakupandisha kwa sijida hiyo daraja, na atakufutia kwa sijida hiyo makosa" Akasema Maadan: Kisha nikakutana na Abuudardaa nikamuuliza, akanambia mfano wa hayo alionambia Thauban.Imepokelewa Imamu Muslim
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «إذا قَام أحَدُكُم من الليل، فَاسْتَعْجَمَ القرآن على لِسَانه، فلم يَدْرِ ما يقول، فَلْيَضْطَجِع».رواه مسلم
Imesimuliwa kutoka kwa Sahal Mwenyezi Mungu amridhie, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Peponi kuna mlango unaoitwa Rayyani, watauingia wafungaji siku ya Kiyama, hato ingia ndani ya Pepo hiyo isipokuwa wafungaji, kutasemwa: Wapo wapi wafungaji? Watasimama hatoingia ndani yake isipokuwa wao, watakapoingia utafungwa kisha hatoingia ndani yake yeyote".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «كان داود -عليه السلام- لا يأكلُ إلا من عمل يده». وعن المقدام بن معد يكرب رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «ما أكل أحد طعاما قط خيرا من أن يأكل من عمل يده، وإن نبي الله داود صلى الله عليه وسلم كان يأكل من عمل يده».حديث أبي هريرة رضي الله عنه: رواه البخاري. حديث المقداد رضي الله عنه: رواه البخاري
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kulikuwa na mtu akiwakopesha watu,basi alikuwa akisema kumwambia kijana wake (Akienda kudai): Ukifika kwa mwenye hali ngumu, basi msamehe, huenda nasi Allah akatusamehe (alipokufa) akakutana na Allah, akamsamehe".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akijitahidi katika siku kumi za mwisho, kwa namna ambayo hakujitahidi katika siku zingine.Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza wazi madhambi, na hakika miongoni mwa kutangaza machafu, ni mtu kutenda dhambi usiku, kisha akaamka akiwa kasitiriwa na Mwenyezi Mungu juu ya dhambi hilo, akaanza kusema: We fulani, jana usiku mimi nilifanya kadhaa wa kadhaa, hali yakuwa alilala usiku kucha Mola wake Mlezi akimsitiri, kisha anaamka asubuhi anafunua pazia la Mwenyezi Mungu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Saad bin Abii Waqas radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Tulikuwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Je anashindwa mmoja wenu kuchuma kila siku mema elfu moja?" Akamuuliza muulizaji miongoni mwa waliokuwa naye kwenye kikao: "Vipi anaweza kuchuma mmoja wetu mema elfu moja?" Akasema: "Atasema Sub-haana llahi mara mia moja (100), kisha ataandikiwa mema elfu (1000), au atafutiwa makosa elfu moja (1000)".Imepokelewa Imamu Muslim
عن ابن مسعود رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «لا حَسَدَ إلا في اثنتين: رجل آتاه الله مالا، فسَلَّطَه على هَلَكَتِهِ في الحَقِّ، ورجل آتاه الله حِكْمَة، فهو يقضي بها ويُعَلِّمَها». وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «لا حسد إلا في اثنتين: رجل آتاه الله القرآن، فهو يقوم به آناء الليل وآناء النهار، ورجل آتاه الله مالا، فهو ينفقه آناء الليل وآناء النهار».حديث ابن مسعود رضي الله عنه: متفق عليه. حديث ابن عمر رضي الله عنه: متفق عليه
عن أبي هريرة ـ رضي الله عنه ـ قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «لا يَلِجُ النارَ رجُل بَكى من خشية الله حتى يَعود اللَّبنُ في الضَّرْع، ولا يَجتمع غُبَارٌ في سبيل الله وَدُخَانُ جهنم».رواه الترمذي والنسائي وأحمد
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kabla ya kufa kwake kwa siku tatu akisema: "Asife mmoja wenu isipokuwa afe katika hali ya kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu"Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Zubair bin Awwam -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Ikiwa mmoja wenu atachukua kamba yake, akaleta mzigo wa kuni juu ya mgongo wake, akauuza, na Mwenyezi Mungu akausitiri uso wake, basi hilo ni bora zaidi kwake kuliko kuwaomba watu wampe au wamnyime"Imepokelewa na Al-Bukhaariy