TopicFiq'hi na misingi yake.
288 hadiths
288 hadiths
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake amesema-: "Ewe baba Saidi, yeyote atakayeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola, na Uislamu kuwa ndiyo dini, na Muhammadi kuwa ni Nabii, basi atakuwa kastahiki Pepo", Abuu Saidi likamshangaza sana hilo, akasema: Naomba uyarudie tena maneno hayo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akarudia, kisha akasema: "Na la mwisho mja ananyanyuliwa kwalo daraja katika Pepo, umbali ulio kati ya daraja mbili hizo ni kama baina ya mbingu na ardhi", Akasema: Ni lipi hilo ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwake na nyumbani kwake kwa daraja zaidi ya ishirini, na hii ni pale mmoja wao atakapo tawadha na akaufanya vizuri udhu, kisha akaenda msikitini hakusudii kwa kwenda kwake ila swala, hakuna kinachomnyanyua isipokuwa swala, basi hatopiga hatua yoyote isipokuwa atanyanyuliwa daraja kwa hatua hiyo, na atasamehewa makosa kwa hatua hiyo mpaka atakapoingia msikitini, na anapoingia msikitini huhesabika kuwa yuko ndani ya swala madamu swala ndio bado inayomzuia kutoka, na Malaika humuombea rehema mmoja wenu madamu akiwa bado kakaa mahala aliposwali, wakisema: Ewe Mola wetu muhurumie, Ewe Mola wetu msamehe, Ewe Mwenyezi Mungu mkubalie msamaha wake, wanaendelea kufanya hivyo kwa muda atakaokuwa hajafanya maudhi yoyote, na madam hajatengua udhu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake