Hadith for the World
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Fiq'hi yaDua na Dhikri mbali mbali.

62 hadiths

62 hadiths

Kutoka kwa Abuu Mussa radhi za Allah ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba yeye alikuwa akiomba kwa dua hii: "Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote, na yale unayoyajua kutoka kwangu, ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu, na yale ya makusudi na ujinga wangu na mzaha wangu, na hayo yote yaliyo kwangu, ewe Mola wangu nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza, wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji, na wewe juu ya kila kitu ni muweza".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiacha dua hizi, kila anaposhinda jioni na kila anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba msamaha na afya katika dini yangu na dunia yangu na familia yangu na mali yangu, ewe Mwenyezi Mungu sitiri uchi wangu -Au aibu zangu- na utie amani yote ninayoyahofia, ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi toka mbele yangu, na nyuma yangu, na kuliani kwangu, na kushotoni kwangu, na juu yangu, na ninajilinda kwa utukufu wako nisijekuvamiwa tokea chini yangu".Imepokelewa na Abu Daud, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
kutoka kwa Abdullahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Ilikuwa miongoni mwa dua za Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa afya yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na kila aina ya hasira zako"Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Abdillah bin Amry bin Aaswi radhi za Allah ziwe juu yao wote wawili yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiomba kwa maneno haya: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui"Imepokelewa na Nasai na Ahmad
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mazuri, na Akhera mazuri, na utukinge na adhabu ya moto".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Shadaad Bin Ausi Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Bwana wa Istighfari (Dua ya kuomba msamaha) Ni kusema: Allaahumma anta Rabbi Laa ilaaha illaa anta, khalaqtani wa anaa abduka wa ana a'laa a'hdika, wawa'dika mastatwa'tu, auudhubika min Sharri maa swana'tu, abuu ulaka bini'matika alaiyya, wa abuu ulaka bidhambi faghfirlii, fa innahuu laa yaghfirudh-dhunuuba illaa anta" Akasema: "Na atakayeisema dua hii mchana akiwa na yakini nayo, akafa katika mchana wake huo kabla hajafika jioni, basi atakuwa miongoni mwa watu wa peponi, na atakayeisema wakati wa usiku akiwa na yakini nayo, akafariki kabla hajafika asubuhi, basi huyo atakuwa miongoni mwa watu peponi".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Maneno mawili mepesi mno katika ulimi, ni mazito mno katika mizani, yanapendeka mno kwa Al-Rahmani (Mwingi wa rehema) Ni: Sub-haanallahil Adhwiim, Sub-haanallaahi wabihamdihi".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Zaidi bin Arqam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Sikwambieni isipokuwa kama alivyokuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kushindwa, na uvivu, na uoga, na ubahili, na ukongwe, na adhabu ya kaburi, Ewe Mwenyezi Mungu ipe nafsi yangu uchamungu wake, na uitakase kwani wewe ndiye mbora wa kuitakasa, wewe ndiye msimamizi wa nafsi na mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyo na manufaa, na moyo usiyo nyenyekea, na nafsi isiyo tosheka, na maombi yasiyo jibiwa".Imepokelewa Imamu Muslim
عن أنس رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان إذا أوى إلى فراشه، قال: «الحمد لله الذي أطعمنا وسقانا، وكفانا وآوانَا، فَكَمْ مِمَّنْ لا كَافِيَ له وَلاَ مُؤْوِيَ».رواه مسلم
عن أبي هريرة-رضي الله عنه مرفوعاً: «اللهم إني أعوذ بك من الجوع، فإنه بِئْسَ الضَّجِيعُ،وأعوذُ بِكَ منَ الخِيَانَةِ، فَإنَّهَا بِئْسَتِ البِطَانَةُ».رواه أبو داود والنسائي وابن ماجه
عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «اللهم إني أعوذ بك من العَجْزِ، والكَسَلِ، وَالجُبْنِ، والهَرَمِ، والبخل، وأعوذ بك من عذاب القبر، وأعوذ بك من فتنة المحيا والممات». وفي رواية: «وَضَلَعِ الدَّيْنِ، وَغَلَبَةِ الرِّجَالِ».متفق عليه. والرواية الثانية رواها البخاري دون مسلم
Kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Sema: Ewe Mwenyezi Mungu niongoze na unisimamie, na kumbuka kwa uongofu ni kuongoka kwako njia, na kusimamiwa ni kusimamiwa kupatia (katika kila jambo lako mithili ya) mshale".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Khaula bint Hakim As-Sulamiyya, amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayeshuka mahali akasema: Audhubikalimaatillaahit-taammaati min sharri maa khalaqa (Najilinda kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyotimia kutokana na shari ya vile alivyoviumba) hakitomdhuru kitu mpaka aondoke mahala pake hapo".Imepokelewa Imamu Muslim
عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: «إذا أوى أحدكم إلى فراشه فَليَنْفُضْ فِرَاشَهُ بِدَاخِلَةِ إزَارِهِ فإنَّهُ لا يدري ما خلفه عليه، ثم يقول: باسمك ربي وضعت جنبي، وبك أرفعه، إن أمسكت نفسي فارحمها، وإن أرسلتها، فاحفظها بما تحفظ به عبادك الصالحين».متفق عليه
عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: «تعوذوا بالله من جَهْدِ البلاء، وَدَرَكِ الشقاء، وسوء القضاء، وشماتة الأعداء». وفي رواية قال سفيان: أشك أني زدت واحدة منها.متفق عليه
عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: كَانَ رَسُولُ اللهِ -صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ- يَقُولُ: «اللهم إني أعوذ بك من البَرَصِ، والجُنُونِ، والجُذَامِ، وَسَيِّئِ الأسْقَامِ».رواه أبو داود والنسائي وأحمد
Kutoka kwa Abdillah Bin Khubaibi Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye amesema: Tulitoka katika usiku wa mvua kubwa na giza nene, tukimtafuta Mtume rehema na amani ziwe juu yake; ili atusalishe, anasema: Nikampata, akasema: "Sema" Nikawa sikusema kitu, kisha akasema: "Sema", Nikawa sikusema kitu, akasema: "Sema" Nikasema: Niseme nini? Akasema: "Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu".Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
عن طلحة بن عبيد الله رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم كانَ إذا رأى الهلالَ، قال: «اللّهمَّ أهِلَّهُ عليْنا بالأمْن والإيمان، وَالسَّلامَةِ وَالإسلامِ، ربِّي وربُّكَ اللهُ، هِلالُ رُشْدٍ وخيرٍ».رواه الترمذي وأحمد والدارمي، وليس عندهم لفظة: "هلال رشد وخير"، وجاءت عند ابن ابي شيبة بسند مرسل
عن جابر رضي الله عنه قَالَ: كُنَّا إِذَا صَعِدْنَا كَبَّرْنَا، وَإِذَا نَزَلْنَا سَبَّحْنَا. عن ابن عمر رضي الله عنهما قالَ: كانَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم وجيُوشُهُ إِذَا عَلَوا الثَّنَايَا كَبَّرُوا، وَإِذَا هَبَطُوا سَبَّحُوا.حديث جابر -رضي الله عنه- رواه البخاري. حديث ابن عمر -رضي الله عنهما- رواه أبو داود
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kusema kwangu: Sub-haanallaah, na Alhamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allaahu Akbaru, kunapendeka sana kwangu kuliko vitu vyote vilizochomozewa na jua".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Ka'b Bin Ujrah Radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Adh-kari za baada ya sala ya faradhi hapati hasara msomaji au mfanyaji wake, kusema Sub-haana llahi mara thelathini na tatu (33), Al-hamdulillahi mara thelethini na tatu (33), Allahu Akbaru mara thelathini na nne (34)".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesoma aya mbili za mwisho wa suratul Baqara zitamtosheleza".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Amri bin Aaswi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili miongoni mwa vidole vya Rahmaan (Mwingi wa rehema), kama moyo wa mtu mmoja, anaugeuza kokote atakako" Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu mwenye kuzigeuza nyoyo, zigeuze nyoyo zetu zielekee katika kukutii".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Abdallahi bin Amru bin A'swi -radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake: Kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, yakwamba yeye alikuwa anapoingia msikitini anasema: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa uso wake mkarimu, na kwa mamlaka yake ya tangu, kutokana na shetani aliyelaaniwa" Akasema: Hivyo tu? Nikasema ndiyo. Akasema: Mtu anaposema hivyo shetani husema: Huyu kalindwa nami siku yake nzima.Imepokelewa na Abu Daud